LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 4, 2019

WAZIRI LUGOLA AMPA MWEZI MMOJA KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akizungumza na Waziri wa Nchi, Wizara ya Amani Demokrasia ya Jamhuri ya Ethiopia, Zeynu Jemal, wakati walipokuwa wanatoka katika Mkutano wa Kimataifa wa Nchi tatu za Afrika, ambazo ni Tanzania, Kenya na Ethiopia, wa kujadili masuala ya Wahamiaji haramu ndani ya nchi hizo. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Diaspora wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kenya, Michael Oyugi.  
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa wa Nchi tatu za Afrika, ambazo ni Tanzania, Kenya na Ethiopia, wakujadili masuala ya Wahamiaji haramu katika nchi hizo. Lugola alimpa mwezi mmoja Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini (CGI), awasake popote walipo madalali wa wahamiaji haramu waweze kukamatwa na kufunguliwa mashtaka nchini. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam, leo Aprili 4, 2019.
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini (CGI), Dk. Anna Makakala, akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa wa Nchi tatu za Afrika, ambazo ni Tanzania, Kenya na Ethiopia, wakujadili masuala ya Wahamiaji haramu katika nchi hizo, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua Mkutano wa Kimataifa wa Nchi tatu za Afrika, ambazo ni Tanzania, Kenya na Ethiopia, wakujadili masuala ya Wahamiaji haramu katika nchi hizo. Lugola alimpa mwezi mmoja Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini (CGI), awasake popote walipo madalali wa wahamiaji haramu waweze kukamatwa na kufunguliwa mashtaka nchini. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, (katikati-waliokaa), Waziri wa Nchi, Wizara ya Amani Demokrasia ya Jamhuri ya Ethiopia, Zeynu Jemal (watatu kulia waliokaa), Mkurugenzi wa Diaspora wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kenya, Michael Oyugi (watatu kushoto waliokaa), na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk Anna Makakala, wakiwa katika picha na wataalamu mbalimbali kutoka Tanzania, Kenya na Ethiopia, mara baada ya kumaliza Mkutano wa Kimataifa wa Nchi hizo uliojadili masuala ya Wahamiaji haramu. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam, leo.(PICHA NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI).

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages