Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Physicians for Human Rights limesema kuwa, watu wasiopungua 60 wameuliwa na maafisa usalama nchini Sudan katika kipindi cha miezi mitatu ya ghasia na maandamano dhidi ya serikali.
Kwa mujibu wa shiriki hilo, vyombo vya usalama nchini Sudan vimeshambulia hospitali na vituo saba vya matibabu katika kipindi hicho cha maandamano, na kuwatia mbaroni madaktari na wafanyakazi wengine wa vituo hivyo 136.
Serikali ya Khartoum inadai kuwa waliouawa katika maandamano hayo ni watu 31 pekee, na wala sio zaidi ya 60 kama yanavyoripoti mashirika huru ya kiraia.
Sudan imekumbwa na maandamano ya kumtaka Rais Omar al-Bashir aachie ngazi tangu katikati ya mwezi Disemba mwaka jana 2018, ambayo chanzo chake kilikuwa ni maandamano hayo kilikuwa ni kulalamikia kupanda bei za bidhaa muhimu hasa mkate na mafuta.
Jana Jumamosi, makumi ya maelfu ya waandamanaji kwa mara ya kwanza tangu maandamano hayo yaanze, waliandamana na kuelekea katika makazi rasmi ya rais na walikusudia kukusanyika pia nje ya makao makuu ya jeshi la nchi hiyo mjini Khartoum.
Polisi iliwakabili kwa mabomu ya kutoa machozi waandaanaji hao waliosikika wakisema "Jeshi Moja, Taifa Moja."
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇