LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 13, 2019

WAPINZANI SUDAN WATANGAZA MASHRTI MATATU YA KUMALIZA MGOMO NA MAANDAMANO YA WANANCHI

Mtandao wa habari wa al Nashra umeripoti habari hiyo na kuwanukuu wapinzani wakisema katika tamko lao la leo Jumamosi kwamba wanataka dhamana ya kukabidhiwa haraka madaraka kwa serikali ya kiraia ya mpito, kufutwa maamuzi yote yaliyochukuliwa kinyume cha sheria na kuondolewa kinga ya kutoshitakiwa viongozi waovu na mafisadi wa utawala uliopinduliwa wa Jenerali Omar al Bashir.
Waziri wa Ulinzi wa Sudan, Luteni Jenerali Ahmed Awad Ibn Auf alikula kiapo cha kuongoza Baraza la Kijeshi la Mpito baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyomng'oa madarakani Omar al Bashir kufuatia maandamano makubwa ya wananchi. Hata hivyo siku moja tu baada ya kuchukua wadhifa huo, Ibn Auf amejiuzulu na kumkabidhi mtu mwingine nafasi hiyo.
Luteni Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan anayeongoza Baraza Kuu la Mpito la Kijeshi nchini Sudan

Aliyechukua uongozi wa Baraza la Kijeshi la Mpito huko Sudan baada ya kujiuzulu Luteni Jenerali Ibn Auf ni Luteni Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan, Mkaguzi Mkuu wa Jeshi la Sudan.
Hata hivyo wananchi ambao wamechoshwa na utawala wa kijeshi huko Sudan wameendelea na maandamano na mgomo wao mbele ya makao ya Komandi Kuu ya Majeshi ya Sudan mjini Khartoum, na idadi yao inazidi kuongezeka.
Wanachoshinikiza wananchi wa Sudan ni kukabidhiwa raia uongozi wa nchi kwa njia za amani baadaye kufanyike uchaguzi huru utakaomuweka madarakani kiongozi aliyechaguliwa na wananchi wenyewe.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages