LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 13, 2019

MKUU WA SHIRIKA LA KIJASUSISUDAN AJIUZULU, MAANDAMANO YAENDELEA

Salah Abdallah Mohamed Saleh, maarufu kwa jina la Salah Gosh, ambaye alikuwa anasimamia Shirika la Kitaifa la Intelijensia na Usalama na ambaye wakati mmoja alikuwa mtu mwenye nguvu zaidi nchini Sudan baada ya al Bashir, analaumiwa kuhusika katika mauaji ya waandamanaji ambao kwa zaidi ya miezi mitatu wamekuwa wakiandamana wakitaka al Bashir aondoke madarakani.
Jenerali Awad Mohamed Ahmad Ibn Auf, Waziri wa Ulinzi wa Sudan aliyetangazwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kijeshi la Mpito baada ya Omar al-Bashir kung'olewa madarakani alijiuzulu jana Ijumaa baada ya waandamanaji kudai mabadiliko zaidi ya kisiasa.
Mkuu mpya wa Baraza la Kijeshi la Mpito Luteni Jenerali Abdel Fattah al Burhan Abdelrahman amekubali kujiuzulu Gosh.

Maandamano ya wananchi wa Sudan

Burhan anatajwa kuwa kamanda wa kijeshi ambaye yuko tayari kuzungumza na waandamanaji. Anatajwa kuwa kiongozi nambari tatu katika Jeshi la Sudan na  amekuwa akisimamia operesheni za askari wa Sudan katika vita vya Saudia dhidi ya wananchi maskini wa Yemen.
Omar Hassan al-Bashir aliyeingia madarakani mwaka 1989 kwa kumpindua kijeshi Sadiq al-Mahdi, ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa wakati huo wa Sudan, alipinduliwa na jeshi la nchi hiyo na kuwekwa kizuizini, baada ya kushuhudiwa maandamano ya wananchi ya kumtaka ang'oke madarakani baada ya miongo mitatu ya utawala wake uliojaa matatizo mengi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages