LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 15, 2019

WAALIMU NCHINI WATANGAZIWA NEEMA

Serikali imesema inaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya kuwalipa walimu na watumishi wengine waliopanda madaraja na stahiki zao ambazo hawajapata kwa muda mrefu licha ya kupanda madaraja.


Hayo yamesemwa bungeni Dodoma na naibu waziri wa TAMISEMI Mwita Waitara akijibu swali lililoulizwa na baadhi ya wabunge la kwanini serikali haitoi malipo stahiki kwa walimu ambao wamewapandisha madaraja kwa mujibu wa taratibu.

Mhe. Waitara amesema tayari serikali imeshatoa maelekezo kwa waajiri wote ikiwemo wakurugenzi wa mamlaka za serikali mitaa kuhuisha barua za kuwapandisha madaraja watumishi ikiwemo walimu  ili waanze  kulipwa malipo yao na kwamba serikali iliamua kusitisha kupandisha madaraja na malipo kutokana na kuhakiki vyeti vya watumishi ili kubaki na watumishi wenye sifa na wanaostahili.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages