LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 15, 2019

IRAN NA OMAN KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIJESHI NA KIULINZI

Kikao cha 15 cha Kamati ya Pamoja ya Ushirikiano wa Kijeshi na Kiulinzi wa Oman na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kimeanza jana mjini Muscut, ambapo pande mbili zimejadiliana njia za kustawisha ushirikiano wao katika masuala ya ulinzi.
Ufunguzi wa kikao hicho umeongozwa kwa pamoja na Brigedia Jenerali Ghadir Nezami, Naibu wa Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Masuala ya Kimataifa na Brigedia Hamad bin Rashid al Balushi, Naibu wa Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Oman Operesheni na Mipango.
Ujumbe wa ngazi za juu wa kijeshi wa Iran unatarajiwa pia kufanya mazungumzo na maafisa wengine wa kijeshi wa Oman katika ziara yao hiyo ya Muscut.

Iran na Oman wakifanya luteka ya kijeshi

Kikao hicho cha 15 kinatazamiwa kumaliza shughuli zake Aprili 18.
Kikao cha 14 cha Kamati ya Pamoja ya Ushirikiano wa Kijeshi na Kiulinzi wa Oman na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kilifanyika hapa mjini Tehran mwezi Mei mwaka jana.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages