LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 17, 2019

UFYATUAJI RISASI SHULE 19 ZAFUNGWA NCHINI MAREKANI

Polisi inamtafuta binti mmoja aliye na umri wa miaka 18 kwa jina la Sol Pais ambaye ametoa matamshi ya kutishia kufyatua risasi katika shule za jimbo hilo. Imesema kutokana na kutoeleweka vyema shule inayolengwa katika tishio hilo, polisi imeamua kufunga kwa muda shule ya sekondari ya Columbine na shule nyingine 18 katika jimbo hilo. Tarehe 20 Aprili 1999 wanafunzi wawili katika shule hiyo walifyatua risasi kiholela na kuwaua wanafunzi 12 na mwalimu mmoja. Polisi ya upelelezi ya FPI imesema kuwa Pais alifika jimboni hapo jana usiku na kwamba tayari alikuwa ameandaa silaha.
Usalama waimarishwa baada ya kutokea ufyatuaji risasi jimboni Colorado
Pais aliwasili katika mji wa Denver, ambao ni mji ulio na wakazi wengi zaidi jimboni hapo na kutoa matamshi ya vitisho, lakini hakusema ni shule gani angeishambulia. Kila mwaka maelfu ya watu katika pembe tofauti za Marekani hupoteza maisha au kujeruhiwa kutokana na ufyatuaji risasi. Ushawishi wa lobi zenye nguvu za utengenezaji silaha katika serikali na kongresi ya Marekani umevuruga juhudi zote zinazofanywa na makundi ya kutetea haki za binadamu zinazolenga kubuniwa sheria kali za kudhibiti umiliki wa silaha nchini humo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages