Rais Recep Tayyip ErdoÄźan wa Uturuki ametaka kuharakishwa mchakato wa makabidhiano ya ngao ya makombora aina S400 wa Russia.
ErdoÄźan ameyasema hayo wakati akirejea katika safari yake aliyoifanya nchini Russia, ambapo amewaeleza waandishi wa habari kwamba kuna uwezekano makabidhiano ya mfumo wa ngao ya makombora wa S400 wa Russia yakafanyika mwezi Julai mwaka huu. Aidha rais huyo wa Uturuki ameongeza kwamba makubaliano ya utekelezwaji wa makabidhiano tayari yamefanyika na kwamba taratibu zote zinazohitajika nazo pia zimefanyika. Hatua ya Uturuki ya kutaka kununua mfumo wa kuzuia mashambulizi ya makombora wa S400 uliotengenezwa na Russia umeizua mgogoro mkubwa kati ya Ankara na washirika wake wanaounda Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi NATO, hususan Marekani.
Kamati ya masuala ya silaha na uhusiano wa kigeni ya bunge la seneti la Marekani Jumanne iliyopita ilitoa onyo kwa serikali ya Ankara kwamba iwapo Uturuki itanunua mfumo huo wa Russia wa kujilinda na mashambulizi ya makombora, basi itawekewa vikwazo na kongresi ya Marekani. Mbali na hayo hivi karibuni pia Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence, aliipa masharti mawili serikali ya Uturuki ya ima kununua mfumo huo wa S400 au ipokonwe uanachama wake katika Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi NATO.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇