LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 11, 2019

RAIS WA SUDAN ALAZIMISHWA KUJIUZULU

  • Taarifa kutoka Sudan zinasema Rais Omar el Bashir wa nchi hiyo amejiuzulu kufuatia maandamano ya miezi kadhaa ya wananchi ambao wamemtaka aachie ngazi baada ya kutawala kwa muda wa miaka 30.
Taarifa kutoka Sudan zinasema jeshi la nchi hilo limemlazimu al Bashir aiuzulu na kwamba Baraza la Mpito linatazamiwa kuchukua madaraka nchini humo. Taarifa kutoka Khartoum zinasema uwanja wa kimataifa wa ndege mjini humo umefungwa huku jeshi likichukua udhibiti wa radio na televisheni ya taifa. Aidha maafisa wa jeshi wamewakamata maafisa wa ngazi za juu cha chama tawala cha National Congress huku Rais al Bashir akiwa katika kifungo cha nyumbani.
Wananchi wenye furaha wameminika katika mitaa ya mji mkuu Khartoum na miji mingine  ya nchi hiyo kusherehekea kuondolewa al Bashir madarakani.  Jeshi la Sudan linatarajiwa kutoa taarifa muhimu kuhusu mustakabali baada ya al Bashir kulazimishwa kujiuzulu.
Waandamanaji nchini Sudan nje ya makao ya Rais al Bashir mjini Khartoum
Maandamano dhidi ya utawala wa al Bashir yalianza mwezi Disemba kulalamikia ughalia wa maisha lakini  baadaye yakachukua mkondo na wigo mpana sasa baada ya vyama vya siasa kujiunga nayo na kutangaza matakwa yao kama kuongezwa uhuru wa kisiasa.
Maandamano ya wananchi wa Sudan yalikuwa ni makubwa kiasi kwamba hayajawahi kushuhudiwa mfano wake katika kipindi cha miaka 30 iliyopita. Waandamanaji walimtuhumu al Bashir na serikali yake kuwa wamevuruga uchumi wa nchi hiyo na wanamtaka yeye na taasisi zote za serikali zing'oke madarakani.
Wananchi wa Sudan walipata msukumo wa kumuondoa al Bashir baada ya wananchi wa Algeria nao kufanikiwa siku chache zilizopita kumuondoa madarakani Rais Abdelaziz Bouteflika aliyetawala nchi hiyo kwa muda wa miaka 20.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages