Waziri wa Ugatuzi Nchini Kenya Eugene Wamalwa amesema wataalamu wametabiri kuwa mvua haitanyesha kwa wakati na kwa msingi huo serikali imeandaa fedha kusaidia kukabiliana na janga hilo.
Wamalwa pia amesema, serikali imetoa dola milioni 6 kununua magunia elfu 26,200 ya mahindi, elfu 17,060 ya maharagwe na elfu 15,420 ya mchele ambavyo vimeshatolewa kwa wahitaji, na dola nyingine milioni 6.8 zimepelekwa kwenye idara ya maji kwa ajili ya kusafirisha maji na kukarabati visima.
Serikali ya Kenya imekanusha taarifa kwamba watu kadhaa wamekufa kutokana na njaa inayosababishwa na ukame ambao kwa sasa umeyaathiri maeno ya kaskazini magharibi mwa nchi hio.
Naye Naibu rais wa Kenya William Ruto amesema Kenya ina uwezo mzuri wa kukabiliana na ukame ikilinganishwa na miaka iliyopita huku akisisitiza kwamba hakuna Mkenya aliyepoteza maisha kutokana na njaa.
Kaunti za Turkana na Baringo ndizo zilizoathiriwa baa la njaa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇