Rais John Magufuli amewataka wakazi wa Njombe kujitafakari kwa matendo yao ya ushirikina yaliyopelekea mauaji ya watoto watano.
Amesema, ni ujinga na kutokuwa na hofu ya Mungu kuamini kuwa utapata mahindi mengi kwa kuua mtoto na kuwaomba viongozi wa Dini na wananchi kwa ujumla kutubu na kumuomba Mungu kwa DOA waliloweka la mauaji.
" Ni doa kwani watoto walitakiwa kwenda shule kwa furaha wanalindwa na kusindikizwa na baba na mama, ninamuomba kiongozi wa aje na sisi sote tutubu mbele ya Mungu." alisema Magufuli.
Rais Magufuli pia alitoa rambirambi ya shilingi milioni Tano kwa familia za watoto waliouawa. Amewataka wakazi wa Njombe kumtanguliza Mungu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇