Na Thabit Hamidu, Zanzibar
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd ameagiza uongozi wa wizara ya Habari, Utalii na mambo ya Kale kuhakikisha wanawapatia haki za wafanyakazi wao wanazozidai na kuwatatulia changamoto zao zinazowakabili.
Alisema kuna baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya habari hususani Shirika la magazeti Zanzibar wamekuwa wakidai stahiki zao kwa muda mrefu hivyo wanatakiwa kupewa ili kuwapa nguvu katika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
“Ni vyema Uongozi wa Wizara Habari, Utalii na Mambo ya kale pamoja na ule Shirika la Magazeti ya Serikali kuhakikisha kwamba haki za fanyakazi wao zinapatikana ili kuwapa nguvu ya kutekeleza majukumu yao kwa nguvu na ufanisi mkubwa” alisema Balozi Seif
Balozi Seif Ali Iddi alitoa agiza hilo wakati akizungumza na uongozi wa Wizara ya Habari, Shrika la Magazeti ya Serikali pamoja na Wafanyakazi wa Gazeti la Zanzibar leo mara baada ya kutembelea ofisi ya Shirika hilo kwa lengo la kujifunza na kujua changamoto zinazowakabili watendaji hao.
Alisema Alisema Viongozi lazima waheshimu mchango mkubwa unaotolewa na Watendaji wao katika utekelezaji wa majukumu yao wakizingatia kwamba Shirika ni muhimu kwa vile linachapisha Gazeti lenye historia kubwa Nchini.
Alisema zipo changamoto kadhaa ambazo zimo ndani ya uwezo wa utekelezaji wa uongozi wa Wizara na Shirika zinazowahusu wafanyakazi hasa maposho ya muda wa ziada na siku ya mapumziko zinazopaswa kushughulikiwa mara moja ili kupunguza au kuondoa malalamiko ya Watumishi hao.
Hata hivyo alisema licha ya changamoto zinazojichomoza kwa wafanyakazi hao katika utekjelezaji wa majukumu yao ya kila siku lakini bado wafanyakazi hao wa gazeti la Zanzibar leo wanapaswa kuepuka mifarakano na mabishano yasiokuwa na msingi ambayo yanaweza kusababisha uzoroteshaji wa kazi zao za kila Siku.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amelipongeza Shirika la magazeti ya Serikali na wafanyakazi wa Zanzibar Leo kwa kazi kubwa ya kuwapasha habari Wananchi juu ya matukio mbali mbali yanayotokea nchini pamoja na nyanja za Kimataifa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇