LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 24, 2019

RAIS MAGUFULI AENDA MALAWI

Rais Dk. John Magufuli leo ameondoka kwenda nchini Malawi ambako kufanya ziara rasmi ya kiserikali ya siku mbili kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo Prof. Arthur Peter Mutharika.

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, imesema, Rais Magufuli akiwa na Mkewe  Mama Janeth Magufuli ameondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, na atapokelewa na mwenyeji wake katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu Mjini Lilongwe.

"Akiwa Mjini Lilongwe Rais Magufuli ataweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu ya aliyekuwa Rais wa Malawi Hayati Bingu Mutharika, kisha atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Mutharika, na jioni atahudhuria Dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa kwa heshima yake na Rais huyo", Taarifa hiyo imesema.

Taarifa imeongeza kuwa kesho Rais Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais Mutharika atamaliza ziara yake kwa kufungua msimu wa Soko la Tumbaku na kuzungumza na wadau wa zao hilo na baadaye atarejea nchini Tanzania ambako ataanza ziara ya kikazi ya siku nane katika Mkoa wa Mbeya.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages