LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 24, 2019

MVUA, MAFURIKO NA MAPOROMOKOYA ARDHI YAUA MAKUMI YA WATU NCHINI TANZANIA NA UGANDA


  • Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika nchi za Afrika Mashariki zimesababisha vifo vya makumi ya watu katika nchi za Uganda na Tanzania.
Watu watatu wamefukiwa na kifusi kwenye Machimbo ya Moram Tanganyika Parkers katika eneo la Moshono jijini Arusha. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shanna amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa, "Watu watatu wameaga dunia katika ajali hiyo ya jana Jumanne iliyosababishwa na mvua zinazonyesha, huku wawili wakiokolewa na kukimbizwa hospitalini."
Huku hayo yakiarifiwa, serikali ya Uganda imesema watu 18 wamethibitishwa kufariki dunia na wengine 100 kujeruhiwa baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko kwenye wilaya za Buyende na Kamuli mashariki mwa nchi.
Msemaji wa polisi wa eneo la Busoga, Michael Kasadha amesema kuwa watu 13 walifariki kwenye wilaya ya Buyende na wengine watano kufariki kwenye wilaya ya Kamuli usiku wa kuamkia jana Jumanne.
Ramani ya Uganda
Wakati huohuo, Idara ya Hali ya Hewa Ufaransa imetahadharisha kuwa, Kimbunga Kenneth kinatazamiwa kutua katika nchi za Tanzania na Msumbiji wakati wowote wiki hii, sambamba na kusababisha mvua kubwa katika kisiwa cha Madagascar leo Jumatano.
Maeneo yanayotazamiwa kushuhudia kimbunga hicho  nchini Tanzania ni Lindi, Masasi, Tunduru na kisiwani Pemba, huku maeneo ya Msumbiji yakitajwa kuwa Marrupu na Montepuez.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages