LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 13, 2019

MWAKYEMB: TUFANYE KAZI KWA KUZINGATIA MAADILI

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Dokta Harrison Mwakyembe ametoa maagizo kwa watumishi wa wizara hiyo kufanya kazi kwa Kuzingatia Maadili na Ueledi wa kazi yao ili kuwaletea Maendeleo Watanzania huku akisisitiza kuwa atakayeshindwa kutimiza wajibu wake hana nafasi .
 
Dokta Mwakyembe ametoa maagizo hayo April 12 ,2019 jijini Dodoma wakati akizindua Baraza jipya la wafanyakazi wa wizara hiyo,hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano Chuo cha Mipango.
 
Dokta Makyembe amewataka watumishi I kutumia nafasi zao katika kutatua kero mbalimbali za wananchi.
 
Aidha Dokta Mwakyembe amezungumzia juu ya tija na Maslahi kwa watumishi ambapo huwawezesha kufanya kazi kwa bidii na kuleta matokeo chanya katika sekta ya Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo.
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa wizara ya Habari ambaye pia ni Katibu mkuu wa Wizara hiyo Bi.Susan Mlawi amezungumzia uboreshaji wa vigezo wa kumpata mfanyakazi bora wa Wizara huku pia akiwatahadharisha watumishi wa wizara hiyo kujihadhari na ugonjwa wa UKIMWI
 
Uzinduzi wa Baraza jipya la wafanyakazi wa Wizara ya Habari, umeenda sambamba na uchaguzi wa viongozi wa Baraza jipya la wizara hiyo pamoja na uzinduzi wa mkataba mpya wa Baraza hilo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages