Na,Enock Magali,Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amefanikiwa kutatua na kumaliza mgogoro wa muda mrefu uliokuwa ukiwakabiri wakazi wa kata ya Chang,ombe eneo la Mtakuja jijini Dodoma.
Kwa mujibu wa mpango wa uendelezaji miji hapo awali eneo hilo lilitengwa kwa matumizi ya ukanda wa kijani yaani "Green belt" wakati huo ikiwa chini ya iliyokuwa Mamlaka ya ustawishaji makao makuu (CDA),na mnamo mwezi Octoba mwaka 2010 viongozi wa dini waliomba sehemu ya eneohilo litumike kwa ajili ya shughuli za mazishi ambapo CDA waliwatengea jumla ya hekari 10 na eneo hilo lilikabidhiwa kwa Manispaa ya Dodoma kwa ajili ya kuanza ujenzi ambapo wananchi walianza kuvamia na kufanya ujenzi holela.
Akizungumza na wananchi wa eneo hilo RC Mahenge amesema ili kuondokana na mgogoro huo Serikali imeamua kuendeleza eneo hilo hivyo wananchi watakao pitiwa na miundombinu Mkurugenzi wa jiji hilo Godwin Kunambi ahakikishe wanapatiwa viwanja mbadala.
Kwa upande wake Mkurugenzi Kunambi amewahakikishia wakazi hao kuwa tayari amekwishaandaa viwanja katika eneo la kikombo ndani ya jiji la Dodoma hivyo kuwataka wananchi hao kujiandaa kisaikolojia kuhamia huko.
Nao baadhi ya wananchi waliohuduhuria katika mkutano huo wamepongeza maamuzi hayo na kusemna kwa ni kweli mgogoro huo umedumu kwa kipindi kirefu ila maamuzi ya Mkuu wa Mkoa yatakuwa ni mwarobaini wa sintofahamu hiyo

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇