LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 7, 2019

MKOA WA KAGERA WAJIPANGA KUBORESHA LISHE MASHULENI

Na Clavery Christian, Bukoba
Idara ya Elimu sekondari katika halmashauri ya Bukoba imesema kuwa imeandaa mkakati utakaosaidia kutokomeza utapia mlo kwa wanafunzi walioko mashuleni na kuandaa kizazi kipya chenye afya bora.

Akizungumza katika kikao cha kamati ya lishe wilayani humo kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo, Chacha Megewa amesema kuwa wanalenga kuboresha huduma za Lishe katika Shule 39 za serikali kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita ifikapo 2021 kwa kuhamasisha jamii juu ya uchangiaji wa lishe kwa wanafunzi wakati wa masomo katika Shule za sekondari.
Amesema kuwa watahamasisha wakuu wa Shule za sekondari kuendelea kupanda miti ya matunda na kuimarisha kilimo cha mboga mboga ili kutoa lishe kwa wanafunzi na walimu na kuongeza kipato cha Shule.

Kwa upande wake Mratibu Wa taasisi ya Agri Thamani Bi. Zaina Rasuli amesema kuwa taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na halmashauri zote za mkoa Kagera kwa kuhakikisha wanatoa Elimu ya kutosha kwa jamii kupitia program zao za kuelisha jamii kwa kutembelea Shule na vituo vya afya na kuongea na wamama wajawazito na wanaonyonyesha kwa kuwapa Elimu ya lishe ili kuondoa tatizo la utapia mlo mkoani Kagera.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages