LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 14, 2019

MAREKANI HUWENDA IKALZIMIKA KUBAKIA SOMALIA BAADA YA 2026

Marekani imedai kuwa inatazamia kukamilisha operesheni zake nchini Somalia ndani ya miaka saba ijayo, lakini iwapo italazimu, vikosi vyake vitasalia nchini humo kwa muda zaidi.
Becky Farmer, msemaji wa Kamandi ya Jeshi la Marekani barani Afrika (AFRICOM) ameiambia kanali ya televisheni ya CNN kuwa, "Mpango wetu ni kusalia Somalia hadi mwaka 2026, lakini huenda tusiwe tumekamilisha operesheni zetu kufikia wakati huo, na hivyo tukalazimika kurefusha uwepo wetu nchini humo."
Amesema Kikosi Maalumu cha Marekani nchini Somalia kilichopewa jina la Danab (radi kwa Kisomali) kina wanajeshi 500 hadi 600, lakini Wizara ya Ulinzi ya US (Pentagon) ina mpango wa kukipanua kiwe na wanajeshi 3000.
Siku chache zilizopita, Rais Donald Trump alisaini dikrii ya kuongeza kwa mwaka mmoja "Tangazo la Rais Kuhusu Hatari ya Kitaifa Somalia, akidai kuwa magenge ya kigaidi katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika yana hatari kubwa na isiyo ya kawaida kwa Marekani.
Marekani ilianzisha mashambulizi ya anga yanayofanywa na ndege zake zisizo na rubani 'drone' nchini Somalia mnamo Juni 2011, lakini hujuma hizo zimeshindwa kulitokemeza kundi hilo la ukufurushaji.




Takwimu za mashambulizi ya anga ya Marekani nchini Somalia 2017

Utafiti uliofanywa hivi karibuni na Taasisi ya Hiraal yenye makao makuu yake mjini Mogadishu ulionesha kuwa, mashambulizi ya anga yanayofanywa kila uchao na Marekani nchini Somalia yameshindwa kulitokomeza au hata kulidhoofisha kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab na badala yake yamekuwa na taathira hasi kwa raia wa kawaida.
Muda mfupi baada ya kuchukua hatamu za uongozi mwanzoni mwaka 2017, Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kuwa Washington itapanua uwepo wa askari wake nchini Somalia.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages