LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 14, 2019

IRAN KUSHIRIKIANA NA UMOJA WA MATAIFA KATIKA ANGA ZA MBALI

Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini Iran Mohammad-Javad Azari Jahromi amekutana na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Anga za Mbali UNOOSA Simonetta Di Pippo ambapo wamejadili masuala mbali mbali ikiw ani pamoja na njia za kukabiuliana na maafa ya kimaumbile na ushirikino katika suala la anga za mbali.
Katika mkutano huo uliofanyika mjini Vienna, Austria, wawili hao wamejadiliana njia za kushirikiana katika kukabiliana na maafa kama vile kiangazi, mafuriko na kulinda misitu.
Waziri wa  Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini Iran na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Anga za Mbali wamejadili kuhusu kufanyika warsha ya kimataifa itakayojumuisha nchi za eneo kujadili matatizo ya mazingira.
Kwa upande wake Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Anga za Mbali UNOOSA Simonetta Di Pippo amesema, moja ya masuala ambayo amejadili na Waziri wa Iran wa Teknolojia na Habari na Mawasiliano ni usimamizi wa majanga ya kimaumbile ambayo Iran inakabiliana nayo.
Halikadhalika amesema wamejadili kuhusu ushirikiano na Iran katika sera na sheria za utumizi wa anga za mbali.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages