LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 11, 2019

KAULI YA SERIKALI KUHUSU CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA AFYA

Serikali imebaini wananchi wanaoishi maeneo ya vijijini wanalazimika kutembea umbali mrefu wa kilometa 119 hadi 300 kupata huduma bora za afya ikiwemo za upasuaji kwa gharama nafuu hali ambayo inachangia wagonjwa wenye kipato cha chini kushindwa kupata matibabu.

Akizungumza wataalamu na wanafunzi wa masomo ya udaktari wa upasuaji kwa njia ya matundu katika hospitali ya rufaa ya KCMC Mkurugenzi wa mafunzo na uendelezaji rasilimali watu wizara ya afya Dkt.Saitore Laizern amesema asilimia 70 ya wananchi wanaoishi vijijini wamekuwa hawapati huduma bora za afya za upasuaji kwa gharama nafuu kutokana na changamoto za upatikanaji wa huduma za afya.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages