LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 12, 2019

JKCI YATAJWA KUTOA HUDUMA KATIKA VIWANGO VYA KIMATAIFA

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imetajwa kutoa huduma katika viwango vya kimataifa na hivyo kupokea wagonjwa kutoka mataifa mbalimbali yakiwemo ya Afrika Mashariki na Kati.

Akizungumza katika kipindi cha ‘TUNATEKELEZA’ Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi amesema kuwa kwa sasa taasisi hiyo ina vifaa vya kisasa vya kutolea huduma ikiwemo mtambo wa kufanyia upasuaji kwa njia ya tundu dogo bila kufungua kifua cha mgonjwa kama ilivyo katika nchi zilizoendelea.

“Kutokana na uwekezaji uliofanywa na serikali katika taasisi yetu kwa mwaka 2018 tuliweza kuwafanyia upasuaji wagonjwa zaidi ya 1400 ambao pengine wangetakiwa kupelekwa nje ya nchi hivyo tumeasaidia kuokoa maisha ya wananchi wengi wenye magonjwa ya moyo” alisisitiza Prof. Janabi.

Akifafanua amesema kuwa jukumu lao kama taasisi ni kuhakikisha kuwa wanatoa huduma bora kwa wananchi na kwa sasa wagonjwa takribani 300 wanahudumiwa katika taasisi hiyo kila siku.

Aliongeza kuwa kwa sasa taasisi hiyo inafanya upasuaji kwa wagonjwa zaidi ya asilimia 85 wanaofika kupata matibabu, lengo likiwa kufikia asilimia 90 kutokana na uwekezaji unaofanywa na serikali ya awamu ya tano.

“Bilioni 5 zimetumika kununua na kusimika mtambo wa kusaidia kufanya upusuajia kwa njia ya tundu dogo” alisisitiza Prof. Janabi

Pia wameanzisha kitengo maalum cha kuhudumia watoto wenye matatizo ya moyo na kufanya uchunguzi kwa watoto wakiwa bado hawajazaliwa ili kuona kama wana tatizo lolote katika moyo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages