Jeshi la Marekani hatimaye limekiri kuwa raia kadhaa wa Somalia waliuawa katika mashambulio ya anga liliyofanya mwaka uliopita wa 2018 nchini humo.
Kwa mujibu wa gazeti la The New York Times, licha ya msimamo wa awali wa jeshi la Marekani wa kukanusha ripoti ya shirika la Msamaha Duniani, Amnesty International kuhusu kuuawa kwa raia wa Somalia katika mashambulio ya anga yaliyofanywa na jeshi hilo mwezi Aprili mwaka jana, hatimaye jeshi hilo limekiri kwamba raia kadhaa wa nchi hiyo ya Pembe ya Afrika walipoteza maisha katika mashambulio hayo.
Kukiri huko kwa jeshi la Marekani kunajiri katika hali ambayo, kamanda wa vikosi maalumu vya Marekani barani Afrika AFRICOM, Jenerali Thomas Waldhaoser ametoa amri ya kuchunguzwa operesheni za anga zilizofanywa na jeshi la nchi hiyo huko Somalia tangu mwaka 2017 hadi sasa.
Hatua hiyo ya ndani ya Marekani imechukuliwa kufuatia mashinikizo ya wabunge na ripoti iliyotolewa mwezi uliopita na shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International ambayo ilieleza kuwa, kuna ushahidi unaoonyesha kwamba, jeshi la Marekani lililifanya mashambulio matano ya anga nchini Somalia, ambapo kwa mujibu wa ushahidi huo makumi ya raia waliuawa katika mashambulio hayo.
Katika ripoti yake hiyo, Amnesty International imetangaza kuwa, vikosi vya jeshi la Marekani vimeongeza kiwango cha mashambulio ya anga nchini Somalia, jambo ambalo limesababisha kuongezeka pia kiwango cha maafa ya roho za raia wa nchi hiyo.../
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇