Msemaji wa polisi wa kijeshi wa Russia walioko nchini Syria ametangaza habari ya kugunduliwa ghala la silaha za magaidi wa Daesh (ISIS) karibu na mji mkuu wa nchi hiyo, Damascus.
Televisheni ya Rusia al Yaum imemnkuu Yusif Mammadov, msemaji wa askari polisi wa kijeshi wa Russia nchini Syria akisema kuwa, ghala hilo limegunduliwa katika kambi ya wakimbizi ya Yarmuk katika viunga vya Damascus. Amesema kuwa, ghala hilo lilikuwa limechimbiwa chini ya ardhi ya nyumba moja, katikati ya majengo mengine ya kambi hiyo ya wakimbizi. Kabla ya hapo pia, jeshi la Syria lilifanikiwa kukamata silaha na zana hatari za kivita zilizotengenezwa na Israel na nchi nyingine za Magharibi hasa Marekani.
Mgogoro wa Syria ulianzishwa mwaka 2011 na maadui wa taifa hilo la Kiarabu ambao walimimina nchini humo magenge mengi ya kigaidi kutoka kona zote za dunia kwa msaada wa Saudi Arabia, Marekani, utawala wa Kizayuni wa Israel na waitifaki wao kwa lengo la kuiangusha serikali iliyochaguliwa kidemokrasia ya Rais Bashar al Assad. Hata hivyo serikali ya Syria kwa msaada wa washauri wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pamoja na msaada wa kijeshi wa Russia imefanikiwa kuwasafisha magaidi wa Daesh nchini humo. Magenge mengine ya kigaidi yanaendelea kumalizwa na kusambaratishwa moja baada ya jingine huko Syria.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇