LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 8, 2019

DC GONDWE KUTUMIA MBIO ZA TANGA CITY KUTANGAZ FULSA ZA UWEKEZAJI NA UTALII

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Godwin Gondwe amesema mkoa huo utaendelea kutumia mashindano ya riadha ya Tanga City Marathon kuweza kutangaza fursa za uwekezaji na utalii zilizopo mkoani Tanga.

Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni ameyasema hayo leo wakati akifunga mashindano ya Tanga City Marathon yaliyofanyika jijini Tanga ambapo msimu huu yameshirikisha washiriki 1,300 kutoka mikoa mbalimbali na nje ya nchi.

Amesema watafanya hivyo kutokana na kwamba mkoa huo kuwa na maeneo makubwa ya uwekezaji yaliyopo mkoani Tanga ili kuweza kuwa vutia kuwekeza kutokana na fursa kubwa zilizopo. “Ndugu zangu tutaendelea kuitumia Tanga City marathon kuweza kutangaza mkoa wa Tanga... Lakini pia kutangaza utalii hata uwekezaji mkoa wa Tanga kwani tuna fursa nyingi sana ambazo mnaweza kuzichangamkia kwenye kufanya uwekezaji “ Amesema.

Pia aliwapongeza washiriki ambao wamefanya vizuri kwenye mashindano hayo na kuwataka kuendelea kujiweka imara kwa kushiriki kwenye mazoezi mara kwa mara ili kuweza kujiandaa na yale yajayo. “Mashindano hayo ya Tanga City Marathon yameufanya mkoa wetu uweze kuendelea kutangazika lakini niwaambie waandaaji wafungue mapema dirisha la usajili msimu ujao “Alisema.

Aidha amesema kwani iwapo watafungua mapema dirisha la usajili wanaweza kupata wadhamini ambao wataweza kuongeza chachu kwenye mashindano hayo msimu ujao. “Pia niwaambie kwamba Mkuu wetu wa Mkoa Martine Shigella anatambua anatambua sana mchango wenu mlijitokeza kushiriki mashindano hayo na sio kwenye michezo pekee anathamini Tanga City Marathon lakini kubwa amenielezea amefurahi kusikia vijana wa shule zetu wameshiriki nao Tanga City Marathon”Amesema.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages