Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) watakaozembea katika kutekeleza ilani ya CCM, hawatapitishwa na chama hicho kugombea tena katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020.
Kauli hiyo imetolewa leo Jumapili Aprili 7, 2019 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole wakati akizungumza katika mkutano mkuu wa jimbo la Sikonge mkoani Tabora.
Polepole amesema ni lazima wabunge watekeleze kwa vitendo ilani ya chama hicho na katika kuweka msisitizo amesema wabunge watakaozembea kutekeleza ilani ya CCM, hawatateuliwa tena
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇