Akiwa katika ziara ya kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020 na akizungumza na wanachama pamoja na Viongozi wa CCM Katika Mkutano wa ndani Kata ya Goba Wilaya ya Ubungo Mkoa wa Dar es salaam Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi amesema Chama Cha Mapinduzi kinawakemea wanachama wake walioanza kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa mapema kabla ya wakati na nje ya utaratibu wa CCM.
Ndg. Polepole ameongeza kwa kusema kuwa CCM imejipanga kushinda kwa kishindo katika uchaguzi wa Serikali za mitaa wa Mwaka 2019 kwani itawaletea wananchi wagombea wazuri wenye sifa na Serikali ya CCM chini ya Rais Magufuli imefanyakazi nzuri ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi katika maeneo mengi nchini.
“Wapo wanachama wameanza kupitapita kwenye wakitaka uongozi nje ya utaratibu wa CCM, niwaambie wanaovunja utaratibu hatutowapitisha” Ndg. Polepole
Wakati uo huo Ndg. Polepole amekagua ujenzi wa madarasa mawili ya kisasa yenye thamani ya Tshs. Milion 39 yanayojengwa na CCM katika Shule ya Msingi Ubungo Kisiwani katika Kata ya Makuburi ikiwa ni sehemu ya Chama kujitoa katika jamii na kuazimisha miaka 42 ya uzawa wa CCM.
Huu ni muendelezo wa ziara za kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa CCM ya Mwaka 2015 – 2020.
Imetolewa na
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇