LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 2, 2019

WAZIRI UMMY ATOA NENO


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ameongelea umuhimu wa uzazi wa mpango na kuwapa nafasi wanawake kushiriki katika maamuzi ya uzazi wa mpango.

Akizungumza jana katika hospitali ya Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro amesema kuwa Wanawake wanatakiwa kupewa nafasi ya kufanya maamuzi ya watoto wanaowataka na kwa kipindi gani.

"Hatuzuii wanawake kuzaa lakini tunataka wanawake wafanye maamuzi wanataka watoto wangapi na kwa kipindi gani ambacho wamepishana." amesema Waziri Ummy.

Huduma za kina mama wajawazito zinazidi kuimarika wilayani Kilosa, huku idadi ya wanawake wanaojifungulia katika vituo vya afya imeongezeka kutoka asilimia75.5 kwa mwaka 2016 hadi 89.2 kwa mwaka 2018.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages