LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 31, 2019

WATU 271 WATHIBITIKA KUAMBUKIZWA KIPINDUPINDU MSUMBIJI


Idadi ya watu walioambukizwa ugonjwa wa kipindupindu nchini Msumbiji imeongezeka mara dufu na kufikia 271,ikilinganaaishwa na idadi iliyotajwa siku moja kabla.

 Hayo yameelezwa na shirika la habari la Ureno, Lusa, likimnukuu mkurugenzi wa kitengo cha taifa cha afya nchini Msumbiji, Ussein Isse.

Hadi sasa hakuna yeyote aliyeripotiwa kufariki kutokana na ugonjwa huo hatari. Katika ripoti nyingine, shirika la habari la Lusa limesema idadi ya watu waliouawa kufuatia kimbunga Idai nchini Msumbiji imefikia watu 501, huku maafisa wa nchi hiyo wakitoa tahadhari kwamba idadi ya vifo itazidi kuongezeka kadri miili ya wahanga wa mafuriko itakavyozidi kupatikana.

Ugonjwa wa kipindupindu umegunduliwa katika mji wenye bandari wa Beira, ambako shirika la madaktari wasio na mpaka limesema kila siku linawaona watu wapatao 200 wenye dalili za ugonjwa huo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages