Mchekeshaji Volodymyr Zelenskiy(41) anaongoza kwa wingi wa kura zinazoendelea kuhesabiwa nchini Ukraine katika duru ya kwanza ya Uchaguzi wa Rais.
Katika kinyang’anyiro hicho yupo pia Rais aliyekuwa madarakani, Petro Poroshenko(53) anayegombea kwa muhula mwingine pamoja na Waziri Mkuu aliyepita, Yulia Tymoshenko(58).
Wagombea hawa ni wale wenye maoni yanayoegemea upande wa Umoja wa Ulaya huku wale wenye maoni yanayoegemea upande wa Urusi wakiangukia pua
Jumla ya wagombea ni 39, ambapo watatu tu ndio wenye matumaini ya ushindi. Endapo hakuna mgombea atakayepata zaidi ya aslimia 50 ya kura, wawili wanaoongoza watachuana katika duru ya pili Aprili 21, 2019
Endapo Zelenskiy atashinda Urais, atakuwa amebadili kipindi chake cha utani ambapo raia wa kawaida anakuwa Rais baada ya kupambana na rushwa kuwa uhalisia
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇