LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 6, 2019

WANACHAMA 14 WASIMAMISHWA UANACHAMA UK

Duru za kuaminika za nchini Uingereza usiku wa kuamkia leo zimetangaza kuwa, wanachama 14 wa chama cha Kihafidhina cha Waziri Mkuu wa nchi hiyo Theresa May wamesimamishwa uanachama kwa tuhuma za kutoa matamshi ya chuki dhidi ya Uislamu.
Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, duru za nchini Uingereza zimemnukuu mwenyekiti wa chama hicho, Brandon Lewis akithibitisha habari hiyo na kuongeza kuwa, uamuzi huo umechukuliwa baada ya Jacob Rees-Mogg, mmoja wa wabunge waandamizi wa chama hicho kusambaza maneno ya chuki dhidi ya Waislamu katika ukurasa wake wa Twitter. Mbunge huyo amesambaza katika ukurasa wake wa Twitter matamshi ya chuki dhidi ya Uislamu ya wanachama wa chama chake cha Kihafidhina.
Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May

Chama tawala cha Kihafidhina cha Uingereza kimewasimamisha uanachama wanachama wake hao 14 wenye chuki dhidi ya Uislamu lakini wakati huo huo hakikutangaza majina ya wanachama hao kinyume na mwenenendo wa kisiasa wa nchi hiyo. Kushindwa kusambaza majina hayo kumewafanya baadhi ya watu waamini kwamba viongozi wa chama hicho ni dhaifu na hawawezi kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu zilizomo kwenye chama hicho.
Kama ilivyo kwa nchi nyingine za Ulaya, Uingereza nayo kutokana na siasa za serikali yake na kuenezwa chuki dhidi ya Uislamu katika vyombo vyao vya habari, mara kwa mara huwa inashuhudia kuzuka magenge ya ubaguzi wa rangi na yenye chuki na Uislamu ambayo yanawashabulia kiadui Waislamu na maeneo yao ya ibada na ya utamaduni.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages