Taasisi ya kimataifa ya utafiti wa masuala ya amani duniani SIPRI imesema uuzaji wa silaha za kivita duniani umeongezeka kwa kiasi cha asilimia nane kwa kipindi cha mwaka 2014 hadi 2018 ikilinganishwa na 2009 hadi 2013.
Kwa mujibu wa taasisi hiyo iliyotolewa leo, Marekani inaongoza kwa kuuza silaha duniani, ambapo imesafirisha zaidi ya theluthi ya silaha katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Marekani imesafirisha asilimia 36 ya silaha zote zilizouzwa kati ya mwaka 2014 na 2018, hiyo ikiwa ni asilimia sita zaidi ikilinganishwa na mwaka 2009 hadi 2013.
Taasisi hiyo yenye makao yake mjini Stockholm, Sweden ambayo pia inachunguza uuzaji wa silaha dunia, imesema Marekani imeuza silaha kwa nchi zipatazo 98 duniani, huku nusu yake zikiwa zimeuzwa katika eneo la Mashariki ya Kati, Saudi Arabia, mshirika wa Marekani ilikuwa soko muhimu zaidi kwa silaha za Marekani, Moja kati ya silaha nne za Marekani ziliuzwa Saudia kati ya mwaka 2014 hadi 2018.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇