Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi akimkabidhi zawadi ya kitabu Mwandishi Mkuu wa Sheria Sarah Kinyamfula Barahomoka katika hafla ya kuwapongeza na kuwaaga watumishi Saba wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao wamestaafu na wanastaafu Utumishi wa Umma. Sarah Barahomoka ambaye anastaafu rasmi mwezi Julai Mwaka huu ni Mwanamke wa Kwanza kuwa Mwandishi Mkuu wa Sheria ( Chief Parliamentary Draftsman) amekuwa katika utumishi wa umma kwa miaka 33.
-------
Na Mwandishi Maalum, Dodoma
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi amesema, Ofisi yake itaandaa utaratibu wa kuwatumia watumishi wake waliostaafu katika maeneo mbalimbali yakimamo ya kufundisha na ushauri.
Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki, wakati wa hafla ya kuwapongeza na kuwaaga watumishi saba ambao wamestaafu na wanastaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria.
Hafla hiyo na ambayo pia ilihudhuriwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Evaristo Longopa ilifanyika katika ukumbi wa Veta Jijini Dodoma
Miongoni mwa watumishi hao wanaostaafu ni pamoja na Mwandishi Mkuu wa Sheria Bibi Sarah Kinyamfula Barahomoka , Mwanamke wa Kwanza kuwa Mwandishi Mkuu wa Sheria tangu Tanzania ipate uhuru na amekuwa katika utumishi wa umma kwa miaka 33 akiwa kaka miaka yote hiyo yote amefanya kazi katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
“Watumishi wenzangu mnaostaafu. Mnastaafu bado mkiwa na akili timamu na afya njema, mnastaafu utumishi wa Umma kwa Heshima kubwa hongereni sana.
Uzoefu mnaoondoka nao hamkuupata kwa mwaka mmoja au mwili, ni uzoefu ambao umejijengea katika kipindi chote cha utumishi wetu” akasema Mwanasheria Mkuu .
Na kuongeza “ Ofisi yangu tutaandaa utaratibu wa kuangaliana namna ya kuutumia uzoefu wenu huu, iwe kwa kutoa ushauri au kwa kuja kufundisha.
Na kwa hiyo msishangae mkiona hata katika ustaafu wenu tunawaomba mje mtusaidie katika kutuongezea nguvu katika maeneo fulanifulani mkiwa kama washauri au wakufunzi.Na ninaomba sana tutakapowaomba na kuwahitaji mtukubalie” akasisitiza na kushangiliwa na watumishi.
Profesa Kilangi amewataka wastaafu hao kwenda na kuutumia uzoefu wao waliojijengea katika utumishi wa umma kwa maendeleo na manufaa yao wenyewe na familia zao lakini pia kwa manufaa na maslani pamana ya Serikali na Nchi kwa Ujumla.
Kuhusu watumishi wate wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Kilangi amewashukuru na kuwapongeza kwa namna ambavyo wameupokea na kuanza kuutekeleza Muundo Mpya wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kufuatia mabadiliko yaliyofanya na Mhe Rais John Magufuli mwaka jana.
“Niwashukuruni sana kwa namna mnavyotekeleza majukumu yenu, wengi wetu tumeyapokea vema mabadiliko ya Muundo wa Ofisi aliyoyafanya Rais mwaka jana na mmeelewa lengo na nia yake ambayo ni kuboresha huduma zinazotolewa na Ofis ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na nipende kusema mbele yenu kwamba sasa ukizungumza na wadau wetu wengi huko nje wanafurahi sana, wanaridhika sana na huduma zinazotolewa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali” akasema .
Pamoja na pongezi hizo, amewataka watumishi wote wa Ofisi yake ni vema wakafahamu ulimwengu wa sasa unahitani watu au watumishi wasomi na wenye uwezo wa juu wa kuelewa mambo na kutatua matatizo na katika muktadha huo ametoa wito wa watumishi wote kila mmoja kwa mujibu wa kada yake kujiendeleza ili Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ikawe kioo na kielelezo bora katika Taifa letu.
“Natoa wito mjiendeleze kwa kulingana na kada zanu mwenye certificate basi apate diploma, mwenye diploma apate degree ya kwanza na mwenye degree ya kwanza apate ya pili na na mwenye ya pili alenge kupata udaktari na hatimaye uprofesa hakuta kuwa na shinda kama ofisi hii itajaa madokta” akasisitiza kwa mkazo.
Pia amewataka watumishi wote kujiandaa kifikra kwa mapokeo ya matumizi ya tehama katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku pamoja na kutumia vema muda wa kazi na kutumia vema raslimali na vitendea kazi vilivyovopo ili kutekeleza vema na kwa tija kauli mbiu ya ‘hapa Kazi tu’
Aidha amesema anaridhiswa na kufurahishwa na idadi kubwa ya watumishi wanawake ambao wameshika nafasi na Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi na Wakuu wa Vitengo utaratibu ambao amesema ameukuta hataka kabla yake.
Akitoa salamu za Shukrani kwa niaba ya wastaafu wenzie Mwandishi Mkuu wa Sheria Bibi Saraha Barahamoka amemshukuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuwaandalia hafla ya kuwapongeza na kuwaaga ikiwa ni pamoja na kuwapatia vyeti vya utumishi.
Akasema yeye binafsi na wenzake wamefurahishwa sana na namna Ofisi ilivyotambua na kuthamini mchango wa utumishi wao katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Serikali na Nchi kwa Ujumla.
Aidha akasema, katika kipindi chote cha utumishi wao katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wamepata ushirikiano mzuri kutoka kwa viongozi wa juu na watumishi wenzao na kwamba wanaomba ushirikiano na moyo huo wa kusaidiana unaendelezwa baina ya viongozi wa wajuu na watumishi wote.
Watumishi wengine waliostaafu ni Bibi Ester James Manyesha ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Uandishi wa Sheria na amekuwa katika utumishi wa umma kwa miaka 35, Bibi Grace Mlondezi Mfinaga, Mwandishi wa Sheria Mkuu Daraja la kwanza na amekuwa katika utumishi wa umma kwa Miaka 36 na Bw. Hussein Shabani Kaweto Msaidizi Kumbukumbu Daraja la kwanza ambaye amedumu katika utumishi wa Umma kwa Miaka 37.
Wengine ni Benadetha Cosman Karadisy ambaye ni Msaidizi wa Mtendaji Mkuu Daraja la Pili na amedumu katika utumishi wa Umma kwa miaka 36, Cosmasi Bayi Machupa ambaye ni Dereva daraja la Kwanza yeye amedumu katika utumishi wa Umma wa miaka 16 na Mary Mahigu Maganga ambaye ni Msaidizi wa Ofisi Mkuu yeye amedumu katika utumishi wa Umma kwa miaka 30
Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao wanastaafu utumishi wa Umma wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya kuwapongeza na kuwaaga iliyoanyika mwisho mwa wiki. miongoni mwa zawadi walizopewa ni pamoja na Kitabu'Retiring Gloriuosly'. Kutoka kushoto na miaka yao ya utumishi kwenye mabano ni Bw. Hussein Shabani Kaweto (37), Bibi Esther James Manyesha (35), Bibi Sarah Kinyamfula Barahomoka (33), Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Evaristo Longopa, Bibi Mary Mahingu Maganga(30), Bibi Benadetha Cosmas Karadisy (36) na Bw. Cosmasi Bayi Machupa (16)
Your Ad Spot
Mar 11, 2019
Home
Unlabelled
AG: TUTATUMIA UZOEFU WA WASTAAFU WETU
AG: TUTATUMIA UZOEFU WA WASTAAFU WETU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇