Tume ya Pamoja ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA imetoa taarifa mwishoni mwa kikao cha 11 mjini Vienna, Austria ikisema kuwa kuondolewa vikwazo ambavyo vinaweza kuboresha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi na nchi hii, ni sehemu ya uhai wa mapatano hayo.
Katika taarifa hiyo, wajumbe wa tume hiyo wamesisitiza udharura wa kutekelezwa kikamilifu na kwa namna athirifu sehemu zote za makubaliano hayo. Kadhalika wajumbe hao wamesisitiza kwamba Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA ni ufunguo muhimu sana katika kuandaa dunia isiyo na silaha za nyuklia kama ambavyo pia ni mafanikio muhimu katika uga wa diplomasia ya pande kadhaa ambayo iliungwa mkono na azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Katika kikao hicho pia wajumbe wa tume hiyo wamepongeza nafasi ya utendaji kazi na isiyo ya upendeleo ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA), ambayo ni taasisi ya pekee yenye wadhifa wa kusimamia na kuunga mkono utekelezwaji wa ahadi zinazohusiana na miradi ya nyuklia ya Iran kupitia azimio hilo.
Taarifa hiyo sambamba na kutaka kuwekwa wazi haraka matokeo yaliyofikiwa, imekaribisha hatua ya kusajiliwa mfumo wa INSTEX kama mfumo maalumu kwa ajili ya kuleta uhusiano athirifu wa kifedha na kadhalika azma ya Ufaransa, Ujerumani na Uingereza kama wahusika wa mwanzo wa kurahisisha biashara na Iran katika kutekeleza sheria na mikataba ya kimataifa na Umoja wa Ulaya. Kikao cha 11 cha Tume ya Pamoja ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA kwa ngazi ya viongozi wa kisiasa na Manaibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na kundi la 4+1 ambazo ni Ujerumani, Uingereza, Ufaransa, Russia na China kilifanyika Jumatano ya jana katika hoteli ya Palais Coburg mjini Vienna, Austria.

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇