Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amesema kuwa hafahamu kama Balozi wa Zambia kama ameshaondoka kwa sababu wamekuwa wanaaga aga mwisho wa siku wakimaliza kuaga watajikuta Ubalozi hawana.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo, Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati akipokea ripoti kutoka TAKUKURU.
"Balozi wa Zambia, sifahamu kama ameshaondoka. Anaenda Zambia tu hapo lakini kila siku anaaga.
Anaaga mara kwa Waziri mkuu, mara sijui ofisi gani, sasa ataaga mpaka kwa wakuu wa mikoa na akimaliza kuaga na ubalozi hakuna," amesema Rais Magufuli.
"Nakupongeza Balozi Mlowola, nenda kafanye kazi, usichelewe kuondoka eti unaaga aga. Nimeshaona hawa Mabalozi nikiwateua kila siku wapo kwenye ofisi wanakwenda kuaga."
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇