Rais
wa Tanzania, John Magufuli amewapongeza kina mama nchini kwa jitihada
mbalimbali wanazozifanya na kwamba waendelee kutembea kifua mbele kwa
kuwa Serikali inawathamini.
Rais Magufuli Awamwagia Sifa Wanawake....Awataka Watembee Kifua Mbele
Rais
Magufuli alitoa kauli hiyo jana Ijumaa Machi 8, 2019 katika uwanja wa
ndege wa zamani wa Julius Nyerere ikiwa ni muda mfupi baada ya kuagana
na Rais wa Rwanda, Paul Kagame aliyekuwa nchini kwa ziara ya siku mbili.
“Nawapongeza
wananchi wote waliojitokeza kumsindikiza Rais Kagame, mmeonyesha
ukarimu wenu kwa Watanzania. Nimefurahi sana kuona kina mama mpo wengi
na leo ni siku yenu.
“Mungu
awabariki mnafanya kazi nzuri sana, endeleeni kuimarisha umoja kwa
Watanzania wote, Serikali ninayoiongoza inathamini sana kazi nzuri
zinazofanywa na kina mama. Endeleeni kutembea kifua mbele na Mungu
atawatunza na mimi sasa hivi nakwenda kumuona mama yangu hospitalini,”
alisema Rais Magufuli huku akishangilia na kina mama waliokuwa uwanjani
hapo.
Mbali
na hilo, Rais Magufuli alivikabidhi Sh1 milioni vikundi vya ngoma
vilivyokuwa vikitumbuiza uwanjani hapo wakati wa hafla ya kuagana na
Rais Kagame.
“Hiki
kidogo mtakwenda kunywa chai. Nawapongeza sana mmekuwa mkionyesha
ukarimu kwa wageni wanaokuja na kupokelewa vizuri,”alisema Rais
Magufuli.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇