Rais Magufuli akizungumza
na Wachezaji wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Taifa Stars ambao walifika
Ikulu mara baada ya kufanikiwa kufuzu kushiriki Fainali za michuano ya Mataifa
ya Africa AFCON baada ya kuifunga Timu ya Taifa ya Uganda The Cranes magoli 3-0
jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli akiwa na
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Naibu Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza, Rais wa TFF Walace Karia,
Bondia wa Ngumi za kulipwa Hassan Mwakinyo wapili kutoka kushoto katika picha
ya pamoja na Wachezaji wa timu ya Taifa
ya Mpira wa Miguu Taifa Stars ambao walifika Ikulu.
Wachezaji
wa Taifa Stars waliopo upande wa kulia pamoja
na viongozi wengine wakionesha ishara ya magoli matatu ambayo timu ya Taifa iliupata
siku ya jumapili dhidi ya Timu ya Uganda The Craines na kufanikiwa
kufuzu kucheza Fainali za michuano ya Mataifa ya Africa AFCON nchini Misri
baadae mwaka huu.
Sehemu ya Wachezaji wa wa timu ya Taifa
ya Mpira wa Miguu Taifa Stars waliopo upande wa kulia pamoja na viongozi
wengine wakiwa katika ukumbi wa Mkutano Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli
akisalimiana na mchezaji wa Timu ya Taifa Taifa Stars Shabani Chilunda
mara baada ya kumaliza kuzungumza na wachezaji hao.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uhamasishaji ya Timu ya Taifa Stars ambaye ni Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda wanne kutoka kushoto waliokaa pamoja na wachezaji wa timu ya Taifa ya Mpira
wa Miguu Taifa Stars waliopo upande wa kulia pamoja na viongozi wengine wakiwa
katika ukumbi wa Mkutano Ikulu jijini Dar es Salaam.
Bondia
wa Ngumi za kulipwa Hassan Mwakinyo kutoka Tanga akijitambulisha Ikulu jijini
Dar es Salaam mara baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza kuhusiana na mafanikio
yake makubwa aliyoyapata katika ngumi za kulipwa pamoja na kuitangaza nchi
kimataifa.
Mfungaji
wa goli la pila la Taifa Stars zidi ya Uganda Erasto Nyoni akijitambulisha
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Bondia
wa Ngumi za kulipwa Hassan Mwakinyo kutoka Tanga akizungumza mara baada ya
kupewa nafasi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli akipiga
makofi wakati Bondia Hassan Mwakinyo alipokuwa akizungumza.
Mchezaji
wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Jonas Mkude akifurahia jambo wakati
wakiwa Ikulu jijini Dar es Salaam pamoja na wachezaji wenzake.
Rais Magufuli
akisalimiana na Kocha wa Taifa Stars Emanuel Amunike mara baada ya kumaliza
kuzungumza na wachezaji wa Timu ya Taifa.
Rais Magufuli
akimsikiliza Mchezaji wa zamani wa Timu
ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Peter Tino ambaye alifunga goli moja
lililoipeleka Tanzania kwa mara ya kwanza katika michuano ya AFCON mwaka 1980
iliyofanyika nchini Nigeria. Pia Rais Magufuli amemsaidia mchezaji huyo wa
zamani kiasi cha Shilingi milioni tano.
Rais Magufuli akiwa
anapata chakula cha mchana na viongozi pamoja na Wachezaji wa timu ya Taifa ya
Tanzania Taifa Stars Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇