Rais Omar al Bashir wa Sudan ametoa amri ya kuwastaafisha maafisa kadhaa wa jeshi la nchi hiyo.
Hatua hiyo ya al Bashir
ilichukuliwa jana Ijumaa ambapo maafisa wengi wa jeshi la nchi hiyo
wamestaafishwa na baadhi yao wamepandishwa vyeo.
Taarifa ya jeshi la Sudan imesema kuwa, maafisa hao wa kijeshi waliopandishwa vyeo ni wa daraja tofauti.
Wakati huo huo jeshi hilo la Sudan limedai kuwa hiyo ni hatua ya kawaida iliyokuwa imepangwa tangu zamani.
Amri hiyo ya kustaafishwa maafisa wa
kijeshi imetolewa na al Bashir katika hali ambayo karibu miezi mitatu
sasa Sudan imekumbwa na maandamano makubwa ya wananchi ambao wanamtaka
al Bashir ang'oke madarakani baada ya kuitawala nchi hiyo kwa miaka 30
sasa.
Taarifa zinasema kuwa makumi ya watu
wameuawa wakiwemo maafisa wa polisi na mamia ya wengine wamejeruhiwa
katika machafuko yaliyotokea kwenya maandamano hayo ya wananchi wa
Sudan.
Wakati huo huo televisheni ya al Jazeera
ya Qatar imetangaza kuwa, kukosekana uongozi maalumu wa wimbi hilo
kubwa la maandamano ya wananchi huko Sudan kunakwamisha mazungumzo baina
ya wananchi hao na serikali.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇