LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 7, 2019

KATIBU MKUU CCM: HAKUNA MWANACHAMA YEYOTE ALIYENUNULIWA KWA PESA


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally amesema kuwa hakuna mwanachama au kiongozi aliyehamia kwenye chama hicho kwa kushawishiwa na fedha.

Akizungumza kwenye kituo cha Televishenu cha TV E amesema kuwa wote wanahamia kwenye chama chao wamekuwa akieleza kuwa wamevutiwa kufanya hivyo.

"Hakuna hata Mwanachama au Kiongozi yoyote alienunuliwa kwa pesa kurudi ama kujiunga na CCM. Wote wamekuwa na maelezo kwamba wamekuwa wanavutiwa na namna CCM na serikali zake wanavyotekeleza ilani zake," amesema.
Dkt Bashiru Ally.

Hivi karibuni CCM walipokea ugeni mkubwa wa Waziri Mkuu Mstaafu,  Edward Lowassa aliyerejea kwenye chama hicho akitokea CHADEMA ambapo alienda mwaka 2015 na kupata nafasi kugombea urais.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages