Mwenyekiti wa kikao kazi ,Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji mkoa wa Arusha Mrakibu Kennedy Komba akizungumza wakati
akifungua kikao kazi leo Jijini Tanga kulia ni Kamanda wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji Mkoani Tanga Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto
Goodluck Zelote
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Tanga Mrakibu
Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto Goodluck Zelote akizungumza wakati wa
kikao hicho kushoto ni Mwenyekiti wa kikao kazi ,Kamanda wa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Arusha Mrakibu Kenedy Komb
Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Tanga Yusuph
Msuya akijitambulisha wakati wa kikao hicho
Sehemu ya wakaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutoka mikoa
ya Kanda ya Kaskazini wakifuatilia kikao hicho
meza kuu wakifuatilia hoja mbalimbali kwenye kikao
hicho
Baadhi ya Askari wa Jeshi la Zimamoto wakifuatilia kikao hicho
Na Mwandishi Maalumu
ASKARI wa Jeshi la Zimamoto na Ukoaji mikoa ya Kanda ya Kaskazini
wametakiwa kufanya kazi kwa waledi,uaminifu na juhudi kubwa
wanapokwenda kuzima moto kwa wananchi ili kuweza kuokoa mali zao na
maisha hivyo kuleta matumaini mapana kwao na jamii zinazowazunguka.
Hayo yalisemwa leo na Mwenyekiti wa kikao kazi ,Kamanda wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Arusha Mrakibu Kenedy Komba kwa Makamanda
wa Jeshi hilo mikoa ya kanda ya Kaskazini kilichokuwa na lengo la
kubadilisha uzoefu na kuona namna ya kutekeleza shughuli zao kwa
ufanisi mkubwa katika kutoa huduma kwa wananchi wa mikoa hiyo.
Alisema anamina baada ya kumalizika kwa kikao hicho kila Kamanda na
mkuu wa kitengo atakuwa amepata faida na kuleta matokeo yaliyomema na
kutukuka kwenye kutoa huduma kwa watanzania mikoa wanayotoka na Taifa
kwa ujumla.
Alisema dhamira kubwa hivi sasa kwao ni kuhakikisha wanaendelea kutoa
elimu kwa wananchi waweze kujua kazi wanayoifanyika hususani
wanapokwenda kuzima moto hivyo wategemee maokozi yatafanyika kwa
juhudi kubwa yawe ya mali au wananchi ili kuleta matumaini mapana kwa
wananchi.
Komba alisema katika kila kazi inapoifanya kwenye sehemu ya kazi
kunapaswa kufanya kazi kwa uaminifu na waledi ili kuwafanya waananchi
wawweze kuwaamini katika utekelezaji wa shughuli zao za kila siku
kupambana na majanga ya moto
“Suala kubwa ni uaminifu na ueledi kwenye kutekeleza majukumu yetu na
tusipofanya hivyo tutapoteza imani kwa weananchi ...tujenge mahusiano
mema na wananchi lakini kubwa zaidi kutekeleza majukumu kwa ufanisi
mkubwa ambao utasaidia kupata wadau walio wema wenye hiari ya
kutusaidia kutupa mawazo kwa sababu ya waledi tunaoufanya “Alisema
“Kila mkoa kuchukua yale mazuri yatakayowasilishwa kwenye kikao hicho
kwenda kuyafanyia kazi ili kikao kijacho kila mkoa uweze kuleta
mafanikiona sio malalamiko kwa kufanya hivyo Jeshi litakuwa la mfano
na kuleta matokeo changa kwa mkoa na Taifa kwa ujumla”Alisema
Alisema hatua hiyo ya kukatana na kubadilisha uwezo wa kazi zao
wanazofanya italeta matokeo changa kwa wananchi wanao wahudumia kwenye
mikoa ya Kanda ya Kaskazini.
Naye kwa upande wake Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani
Tanga Yusuph Msuya alisema dhani ya idara ya ukaguzi ni kupunguza
majanga kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye majengo, magari ili
kuwawezesha watumiaji kuepukana nayo.
Alisema mpaka sasa wamekwisha kufanya kwa vyombo vya moto vipatavyo
384 ambapo kati ya hivyo mabasi 235 hali zao ni nzuri na yaliyosalia
tumewapa ushauri namna ya kufanya ili waweze kuondokana na mapungufu
yaliyobainika.
“Ukaguzi tulioufanya kuanzia mwezi Desemba mpaka sasa kwa vyombo 384
kati ya hivyo mabasi 235 hali zao ni nzuri na yasiyosali tumewapa
ushauri ili waweze kuondoa mapungufu yaliyobainika”Alisema
Your Ad Spot
Mar 22, 2019
Home
Unlabelled
ASKARI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WALEDI
ASKARI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WALEDI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇