Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kawaida wa 20 wa Viongozi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha Februari 1, 2019. Katika mkutano huo viongozi hao wamekubaliana mazungumzo ya kutatua mgogoro wa kisiasa nchini Burundi yaendelee, na wakati huo huo Rais Kagame amekabidhiwa uenyekiti wa Jumuiya hiyo. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi Mhe. Gaston Sindimo alipowasili katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) kuhudhuria Mkutano wa Kawaida wa 20 wa Viongozi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha Februari 1, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudani ya Kusini Mhe. Barnaba Marial Benjamin akiwa na Balozi wa Nchi hiyo nchini Mhe. Mariano Deng Ngor wakati alipowasili katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) kuhudhuria Mkutano wa Kawaida wa 20 wa Viongozi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha Februari 1, 2019.
Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame akilakiwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Liberat Mfumukeko na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakati alipowasili katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) kuhudhuria Mkutano wa Kawaida wa 20 wa Viongozi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha Februari 1, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kawaida wa 20 wa Viongozi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha Februari 1, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta alipowasili katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kawaida wa 20 wa Viongozi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha Februari 1, 2019.
Rais wa Uganda Mhe. Yowweri Kaguta Museveni akilakiwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Liberat Mfumukeko na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakati alipowasili katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) kuhudhuria Mkutano wa Kawaida wa 20 wa Viongozi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha Februari 1, 2019.
Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) wakihudhuria Mkutano wa Kawaida wa 20 wa Viongozi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha Februari 1, 2019. (PICHA NA IKULU)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇