LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 2, 2019

MAREKANI YAJIONDOA RASMI ' KWA MUDA' KATIKA MKATABA WA INF

Serikali ya Marekani imetangaza rasmi kusimamisha kwa muda utekelezaji wa mkataba wa Silaha za Nyuklia za Masafa ya Kati (INF).
Akitangaza uamuzi huo hii leo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo amesema yumkini Washington ikarejea katika mkataba huo katika muda wa siku 180, iwapo Russia itatekeleza matakwa ya Marekani. 
Serikali ya Moscow imeeleza kusikitishwa kwake na kitendo hicho cha Marekani kujiondoa kwa muda kwenye mkataba wa Silaha za Nyuklia za Masafa ya Kati (INF).  Msemaji wa Ikulu ya Russia (Kremlin), Dmitry Peskov amesema, Marekani inaituhumu Moscow kwamba imekiuka mkataba wa INF, lakini haijatoa nyaraka wala ushahidi wowote wa kuthibitisha tuhuma hizo, na kwamba uamuzi huo wa kujiondoa ulifikiwa kitambo sana.
Hivi karibuni Rais Vladimir Putin wa Russia, alionya kuwa, kujitoa Marekani katika mkataba wa Silaha za Nyuklia za Masafa ya Kati kutailazimisha Moscow nayo kujibu mapigo.
Russia imesema inapinga kuvunjwa mkataba wa INF, lakini endapo hilo litatokea, itatoa jibu kwa njia mwafaka.
Kabla ya hapo pia Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani alikosoa uamuzi huo wa Marekani wa kujitoa katika mktaba wa INF na kuyataja makubaliano hayo kuwa miongoni mwa mikataba muhimu sana ya kudhibiti silaha za nyuklia.
Makubaliano hayo ya pande mbili ya kutokomeza Silaha za Nyuklia za Masafa ya Kati (INF) yalisainiwa mwaka 1987 na viongozi wa wakati huo wa Marekani na Shirikisho la Kisovieti la Urusi ya zamani, na kutajwa kama hatua muhimu ya kuondoa hali ya mivutano katika enzi hizo za Vita Baridi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages