LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 2, 2019

UN YASIKITIKA KUFUNGWA MAISHA JELA VIONGOZI WA UPINZANI BAHRAIN

Umoja wa Mataifa umetilia shaka mchakato wa kesi, baada ya mahakama ya Bahrain kuwahukumu kifungo cha maisha jela viongozi wa upinzani nchini humo.
Marta Hurtado, msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa amesema, "Tuna wasiwasi mkubwa kuwa hukumu zilitolewa dhidi ya viongozi hao zilitokana na misimamo yao dhidi ya serikali na sera zake."
Amesema UN inatilia shaka pia mchakato wa kesi dhidi ya shakhsia hao wa kidini na kisiasa, na yumkini haki yao ya kufanyiwa uadilifu katika kesi dhidi yao imekiukwa.
Siku chache zilizopita Mahakama ya Juu ya Bahrain iliidhinisha kifungo cha maisha jela dhidi ya shakshia watatu mashuhuri wa kidini na kisiasa nchini humo, akiwemo Sheikh Ali Salman, ambaye ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya al Wifaq.
Sheikh Ali Salman wa Bahrain
Aidha wanachama wawili wa ngazi za juu wa harakati hiyo iliyopigwa marufuku na watawala wa Manama, Hassan Sultan na Ali al Aswad, walihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa tuhuma zisizo na msingi kwamba walikuwa wakifanya ujasusi kwa niaba ya Qatar. 
Mapema wiki hii Umoja wa Ulaya na shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International ziliutaja uamuzi huo wa vyombo vya mahakama vya Manama kuwa pigo jingine kwa uhuru wa kujieleza nchini Bahrain.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages