Chuck Schumer, Kiongozi wa Walio Wachache katika Bunge la Seneti nchini Marekani ameashiria maneno ya kitoto na kipuuzi ya Rais Donald Trump wa nchi hiyo kuihusu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kumtaka rais huyo arudi darasani akafundishwe tena.
Katika radiamali yake kuhusiana na uelewa jumla wa kitaarifa wa rais huyo, Chuck Schumer amemtaka Dan Coats, mkuu wa kitengo cha intelejensia, Gina Haspel, mkuu mpya wa Shirika la Kijasusi la Marekani CIA na Christopher A. Wray, mkuu wa Polisi ya Federali (FBI) ya nchi hiyo kumpa ukweli na kumfundisha taarifa sahihi Trump kuhusiana na namna sahihi ya kuamiliana na hali ya Iran. Aidha Kiongozi wa Walio Wachache katika Bunge la Seneti nchini Marekani amesema: "Hamuwezi kuruhusu kutolewa matamshi ya kipuuzi na yasiyo sahihi ya leo ya Trump kama rais wa Marekani na ni lazima mumfundishe ukweli na misingi ya awali ya taarifa jumla." Amesema Chuck Schumer.
Kadhalika Schumer amebainisha kwamba Rais Donald Trump anatumia taarifa jumla katika maeneo yasiyofaa na hivyo kutoa pigo kwa Marekani yenyewe na kwa ajili hiyo kuna haja kutafutwe njia ya kumuelekeza rais huyo wa Marekani. Baada ya kutolewa taarifa mpya ya hivi karibuni kwamba Iran haina lengo la kuunda silaha za nyuklia, rais Donald Trump sambamba na kupinga taarifa hiyo aliwataja viongozi wa intelejensia wa nchi hiyo kuwa wepesi na wasiojua mambo na kwamba huenda ikahitajika wataalamu hao kurudi shuleni.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇