LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 12, 2019

UN: MAPIGANO MAPYA SUDAN KUSINI YASABABISHA WATU 13,000 KUWA WAKIMBIZI

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema mapigano mapya yaliyoibuka nchini Sudan Kusini yamesababisha watu 13,000 kuwa wakimbizi ndani na nje ya nchi.
UNHCR imesema mapigano hayo yaliyoibuka tarehe 19 mwezi uliopita kati ya wanajeshi wa serikali ya Sudan Kusini na magenge ya waasi yamesababisha maelfu ya watu wakimbilie usalama wao katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Amesema aghalabu ya wakimbizi hao waliwasili kwa miguu katika vijiji vya mkoa wa Ituri kaskazini mashariki mwa DRC mwishoni mwa wiki wakitokea Sudan Kusini, na kwamba waliingia katika nchi hiyo jirani kupitia mji wa mpakani wa Ingbokolo.
Taarifa ya leo Jumanne ya UNHCR imesema watu wengine elfu nane wamelazimika kuwa wakimbizi wa ndani katika mji wa Yei, kusini magharibi mwa Sudan Kusini kutokana na mapigano hayo mapya.
UNICEF: Wanawake na watoto ndio wahanga wakuu wa mapigano Sudan Kusini
Mapema mwezi huu wa Februari,  watu tisa waliripotiwa kuuawa katika wimbi hilo jipya la mapigano katika jimbo la Amadi, magharibi mwa nchi hiyo changa zaidi barani Afrika.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Manasseh Dobuyi, Naibu Gavana wa jimbo la Amadi, askari saba na raia wawili waliuawa katika mapigano hayo ya kati ya askari watiifu kwa kiongozi wa upinzani Riek Machar (SPLM-IO) na wapiganaji wa National Salvation Front (NAS) inayoongozwa na Jenerali Thomas Cirillo.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages