Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii inatarajia kuanza mkakati maalumu wa kuongeza idadi ya watalii wenye umri mkubwa kuanzia miaka 50 na kuendelelea.
Pia, mkakati huo utalenga kundi la watalii wenye bima za maisha zinazowaruhusu kusafiri na ndege kubwa zenye rubani wawili zitakazotua moja kwa moja kwenye Hifadhi pamoja na wale wasioweza kusafiri kwa njia ya barabara kwa muda mrefu.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu wakati alipokuwa akizungumza na Menejimenti ya Uongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro katika ziara yake ya kikazi wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.
Akibainisha mikakati hiyo, Naibu Waziri huyo ameutaja mkakati wa kuanzisha magari yatakayokuwa yakitembea kwenye waya (Cable cars) kwa ajili ya kutumiwa na watalii wenye umri mkubwa kuanzia miaka 50 kupanda Mlima Kilimanjaro ambao kutokana na umri wao hawawezi kupanda kwa njia ya kawaida.
Amesema kama nchi imekuwa ikikosa pesa nyingi zinazotokana na watalii wa kundi hilo ambao ndo wengi wanaokuja nchini kwa ajili ya kutalii mara baada ya kustaafu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇