Jumba refu la Britam Tower lililopo jijini Nairobi nchini Kenya limepokea tuzo inayopewa majumba marefu duniani ya Emporis Skyscraper Award.
Ni jumba la pekee barani Afrika kushiriki katika tuzo hiyo miongoni mwa majumba 10 bora duniani katika historia ya tuzo hiyo ya miaka kumi na tisa.
Hatua hiyo inalifanya jumba hilo lililojengwa na kampuni ya Britam Properties Limited kuwa jumba refu zaidi katika eneo la Afrika mashariki na kati , likiwa na urefu wa mita 200.
Britam Tower lilichunguzwa pamoja na mengine mengi barani Ulaya, Asia na Marekani ambayo yalishirikisha Generali Tower mjini Milan, jumba la Chicago's 150 North Riverside na lile la Riverpoint.
Nafasi ya kwanza ilichukuliwa na jumba la Lotte World Tower mjini Seoul, Korea Kusini. Tuzo ya The Emporis Skyscraper ni tuzo maarufu duniani miongoni mwa ujenzi wa majumba marefu.
Washindi huchaguliwa na jopo la wataalam wa usanifu kutoka kila pembe duniani , huku majumba yelioteuliwa kuwania tuzo hiyo yakishinda kwa vigezo vya mvuto na ufanisi wao.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇