LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 20, 2019

RUGE MUTAHABA NDIYE ALIYE NISHAURI KUTEMBEA PEKU



Msanii wa mashairi nchini, Mrisho Mpoto amesema mtindo wake wa kutembea bila viatu ulikuja baada ya kushauriwa kufanya hivyo na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media, Ruge Mutahaba.

Mpoto ametoa siri hiyo wakati akihojiwa na mtangazaji katika kipindi cha Clouds 360 kwenye Kituo cha Televisheni cha Clouds TV na kuongeza kuwa Ruge pia amechangia sana kumtengeneza kisanaa.

"Aliniambia tayari wewe unaimba mashairi je unataka watu wakupambanuaje?, nikamwambia nitavaa magunia akasema sawa hiyo haitoshi ongezea nyingine”

Ameendelea kwa kusema kuwa, 'Ni Ruge aliyenitengeneza mimi kuwa tofauti kwa mashairi yangu, mwanzoni nilikuwa naimba tu kikubwa zaidi alinitengeneza yaani kuni-brand,'

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages