LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 28, 2019

MWENYEKITI WA CUF MWANZA ATIMKIA CCM

Mwenyekiti wa Mtaa wa Jiwe Kata ya Igogo Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza kwa tiketi ya chama cha  Civic United Front (CUF) Salehe Bilali ameachia ngazi katika chama hicho na kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM). 

Akizungumza na CCM Blog, Bilal (Pichani), amesema kwamba amehamia rasmi CCM Februari 10, 2019, baada ya kuitumika CUF kwa zaidi ya miaka 25 kama muasisi.

Alisema akiwa CUF alikuwa akifanya jitihada za kutatua kero mbalimbali zinazo wakabili wananchi kwa kuhakikisha  zinapatiwa ufumbuzi. 

"Nikiwa Mwenyekiti wa mtaa wa Jiwe, nimeweza kufuta kero mbalimbali katika mtaa wangu na kupambana kutetea maendeleo ya wananchi wangu katika Mtaa wa Jiwe.

Leo hii kero ya uporaji, uvunjaji majumba kwa kutumia jiwe maarufu la fatuma, vyote vimekwisha, nimepigana huduma za maji mashuleni na kwenye zahanati na umeme leo wapo wanasambaza nguzo za umeme na nimekwisha waandikia Tarura na barua waweze kutuwekea Barabara kwa kiwango cha mawe" alisema Bilali.

Kwamba kwa kuwa Rais Dk. Jonh Magufuli amekuwa mstari wa mbele katika kutetea na kuboresha maisha ya wananchi anakubaliana naye na hivyo hana budi kumuunga mkono ili kuongeza nguvu katika mtaa wake. 

Bilali ameongeza kuwa ni imani yake kwamba akiwa ndani ya Chama cha Mapinduzi itakuwa rahisi zaidi kuwaletea maendeleo wananchi wa mtaa wa Jiwe

Amewaomba wanachama wa CCM kumpa ushirikiano kwa kumuunga mkono kwani amerudi nyumbani kwa kuwa kabla ya kwenda CUF alitokea CCM.

Alisema katika CUF  amewahi kushika nyadhifa mbalimbali kama Mwenyekiti wa Tawi, Mweka hazina wa Kata, Mjumbe Kamati ya utendaji ya wilaya ya Nyamagana, Mwenyiki wa  kata wa Chama cha CUF Kata ya igogo,  na kuwa mjumbe wa Chama cha michezo wa mpira wa miguu wilaya ya nyamagana ndani ya miaka kumi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages