LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 5, 2019

MWENYEKITI WA CCM RAIS DK. MAGUFULI AAHIDI KUKIPA SH. MILIONI 200 KITUO CHA TELEVISHENI CHA CHANNEL TEN

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk. John Magufuli akimsikiliza mtayarishaji vipindi wa kituo cha Televisheni cha Channel Ten Abdalaah Lugisha alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na CCM, ikiwa ni sehemu ya shuguli alizifanya kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM, Jijini Dar es Salaam, leo Febuari 5, 2019. 
-------------
DAR ES SALAAM
Mwenyeki wa CCM, Rais Dk John Magufuli ameahidi kutoa sh. Milioni 200 ndani ya siku mbili kwa ajili ya kununulia vitendea kazi vya kituo cha Televisheni cha Cannel ten ili kuboresha huduma zake.

Rais Magufuli ametoa ahadi hiyo leo alipotembelea Ofisi za Kampuni ya Media Group Ltd (AMGL) inayoendesha vituo vinne vya televisheni kikiwemo Channel ten na vituo viwili vya radi kiÄ·iwemo cha Magic fm ambapo pamoja na ahadi hiyo amewataka wafanyakazi wa Kampuni hiyo kumpelekea mapendekezo ya jengo lolote la CCM lenye hadhi nzuri ili kuhamishiwa kituo hicho.

Aidha, Rais Magufuli amewapongeza wafanyakazi hao kwa kazi nzuri wanazozifanya na amesema kuwa dhamira yake ni kuhakikisha kituo hicho kinaboreshwa, matangazo yake yanafika maeneo mengi ya ndani na nje ya nchi na kinakuwa kituo cha mfano kwa vituo vingine hapa nchini.

Pia amewataka wafanyakazi hao kujenga umoja wa dhati, kuchapa kazi kwa juhudi zaidi ili kuongeza uzalishaji wa mapato na kuzalisha maudhui ambayo yatawasaidia Watanzania kupata manufaa kama vile kutoa elimu ya kilimo, biashara, ufugaji na uvuvi.

“Nataka Africa Media Group Ltd iwe na vyombo vyenye nguvu, vinavyotazamwa kila mahali hapa nchini hadi nje ya nchi, Tanzania haiwezi kuwa soko la kuangalia vyombo vya habari vya kutoka nje ya nchi, watu waangalie vyombo vya habari vya nje lakini vyombo vyetu viwe ndio mwongozo wa maisha ya Watanzania zaidi ya Milioni 50.

“Na hii natoa wito kwa vyombo vyote vya Tanzania, mna wajibu wa kuzungumzia mazuri ya Tanzania, lakini pia muendelee kutoa elimu kwa Watanzania, Watanzania karibu asilimia 75 ni wakulima, toeni vipindi vya kuonesha kilimo bora, ufugaji bora, nakadhalika” amesema Rais Magufuli.

Baada ya kutoka AMGL, Rais Magufuli amekagua mradi wa ukarabati mkubwa wa jengo la kitega uchumi la CCM (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba Jijini Dar es Salaam ambalo litakamilika mwezi Juni mwaka huu, na akiwa nje ya jengo hilo amesalimiana na wananchi wakiwemo wafanyabiashara ndogondogo ambao amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kutimiza wajibu wake wa kuwapigania Watanzania wote bila kubagua.

Rais Magufuli amemalizia ziara yake kwa kutembelea Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba Jijini Dar es Salaam na kuzungumza na wafanyakazi ambapo amewahakikishia kuwa chama chao (ambacho ni chama tawala) kinakwenda vizuri hasa baada ya hatua zilizochukuliwa kusimamia misingi ya chama, mali na mapato ya chama, maadili na uongozi na pia kurejesha mali za chama zilizokuwa mbioni kupotea.

Rais  Magufuli ameoata fursa ya kuzungumza na wanachi kwa nyakati tofauti, ambapo amewahakikishia Watanzania wote kuwa Taifa linakwenda katika mwelekeo mzuri hasa baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha uchumi na huduma za kijamii kama vile afya, elimu, maji, nishati na miundombinu ya usafiri.

Akiwa Mtaa wa Zanaki, Wilaya ya Ilala,  baada ya kutembelea kampuni ya AMGL ambayo kwa sasa inamilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Magufuli amesema pamoja na mafanikio hayo, Serikali itaendelea kupambana na dhuluma na matumizi mabaya ya rasilimali za Taifa na ametoa mwito kwa Watanzania wote kuiunga mkono kwa kuhakikishia wanatanguliza maslahi ya Taifa. PICHA KEMKEM ZA ZIARA HIYO>BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages