Mashindano ya soka la mchangani kwa vijana wanaume na mashindano ya mpira mstari kati kwa wasichana, ni miongoni mwa michezo kwenye mashindano hayo ambayo yameonyesha msisimko mkubwa kwa wananchi wa rika zote kujitokeza kuishuhudia kila siku tangu ilipoanza Februari 3, 2019.
Mashindano hayo yameonyesha kuwa na mvuto kutokana na kuwa ya aina ya kipekee kwa waandaji kuamua kuyafanyia mitaani badala ya kutumia viwanja vya michezo au vya wazi kama ambavyo imekuwa ikifanyika kwa michuano mingi.
Mvuto mwingine kwenye mashindano hayo ni kuamliwa kutumika vifaa vya kinyumbani nyumbani ambapo mipira inayotumika katika soka na mstari kati ni ya kutengenezwa kwa mikono na nyavu za kwenye magoli wameamua kutumia vyandarua chakavu.
"Mashindano haya ni ya vijana wa CCM Tawi la Malapa katika kusheherekea CCM kutimiza Miaka 42, pmoja na vijana wenyewe, mashindano haya yamedhaminiwa na Chamä cha Mapinduzi tawi la Malapa, Viongizi na makada wa CCM katika tawi hili la malapa ambao kwa pamoja wamesapoti zawadi huku Vijana wakibeba jukumu la usimamizi wa mashindano hayo.
Mashindano yatakuwa endelevu katika kufanya kazi za Chama ndani ya umma ili kuwavutia Vijana wengi kuiunga mkono CCM, hatimaye kushinda uchaguzi wa mtaa mwaka huu na uchaguzi mkuu 2020 ikizingatiwa mtaa wetu huu wa Malapa upo upinzani kwa miaka 15 sasa na Kata ya Buguruni ulimo mtaa huu ipo upinzani kwa miaka mitano sasa", alisema Aluu Segamba ambaye ni Kada wa CCM na mkazi wa mtaa huo wa Malapa. Msikilize Mwenyekiti wa UVCCM TAWI LA MALAPA> BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇